Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 8 Machi 2015

MKILANIA.COM Diamond Platinumz Akaliwa Kooni na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

MKILANIA.COM Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imemtaka meneja wake kutoa nyaraka zinazoonyesha Mikataba ya Diamond ndani ya siku saba (7).
Inaelekea kuna jambo haliko sawa!

Jumamosi, 7 Machi 2015

MKILANIA.COM Ukweli wa Snura Kujifungua Wajulikana.. Mwenyewe Akubali Kudanganya Watanzani

MKILANIA.COM Wiki chache zilizopita tuliweka story kuhusu msanii Snura kujifungua na akakana kua hajajifungua na tukaweka story kuhusu mwonekano wake mpya baada ya kufungua japo alikana kua hakua amezaa mtoto
Sasa mpya ya leo ni story ya Snura kukubali kua ni kweli alizaa na baba wa mtoto huyo ni Dj wa Maisha Club Dj Hunter. Kitu cha kwanza Snura kufunguka ni sababu iliyomfanya yeye kuficha taarifa hizo za ujauzito na snura alisema kuasababu ya yeye kuficha kuwa ana mimba na kuficha kuwa ana mtoto sio sababu ya kuogopa walimwengu bali sababu za kikazi alijua mapromota ukisema una ujauzito hawakupi kazi,yeye ndio baba na mama wa watoto wake so aliangalia zaidi maslahi na alipiga mzigo mpk mimba ina miezi 5,alipoona sasa hawez tena walipanga na meneja wake waseme kaenda south kufanya video kumbe alikuwa chumbani kwake.
Snura alijifungulia hospitali ya Palestina Dar na wakati anaenda alivaa baibui kininja na aliwaomba manesi ajifungue chumba cha pekeyake. Snura kwa sasa yupo fit kupiga mzigo na ndio maana kayaweka wazi ana mtoto wa kiume anaitwa Taltham..

Alhamisi, 26 Februari 2015

MKILANIA.COM Waliomuiba Albino Pendo Wakamatwa Mwanza

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
MKILANIA.COM Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amesema watu wote waliohusika ‘kuiba’ mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino) Pendo Emmanuel (4) katika kijiji cha Ndami wilayani Kwimba, Mwanza, wamekamatwa.

Akizungumza wakati akiwaapisha wakuu wapya wa wilaya wa mkoa huo jana, Manju Msambya (Misungwi), Zainab Rajab (Sengerema) na Pili Moshi (Kwimba), Mulongo alisema watu wote waliohusika wamekamatwa na hivi sasa bado hawafahamu kama mtoto huyo yupo hai ama mfu.
“Wezi wale baada ya kumuiba mtoto Pendo walimleta katika hoteli moja hapa jijini Mwanza, kisha kuwakabidhi watu walionekana wanunuzi, lakini wote hao wamekamatwa akiwamo mmiliki wa hoteli hiyo,” alisema Mulongo.
Alisema serikali ipo kazini wakati wote, ndiyo maana inafanya kazi usiku na mchana kuwasaka watu wote waovu mkoani Mwanza ambao hawawezi kusalimika kwa kile watakachokifanya.
Hata hivyo, alisema watu hao waliofanya uhalifu huo akiwamo baba wa mtoto huyo, Emmanuel Shilinde, wanashikiliwa na polisi huku mtu wa mwisho aliyetoweka na mtoto huyo toka hotelini hapo akiendelea kutafutwa.
Mulongo hata hivyo hakuweza kuitaja hotel wala mmiliki wake na wangine waliohusika na tukio hilo lilitokea Desemba 27 mwaka jana, lakini Shilinde akituhumiwa kuhusika zaidi na tukio hilo kutokana na kuamua kufanya hivyo kwa sababu alikuwa ana watoto wawili albino.
Mkuu wa mkoa huyo aliwataka wakuu wa wilaya wapya, kuhakikisha kushughulikia changamoto za wapiga ramli, kuangalia utoaji wa vibali kwa waganga wa jadi ili kudhibiti matyukio ya utekaji na mauaji ya albino.
Hata hivyo, alishangazwa na maneno yanayotolewa na watu kuhusiana na mauaji hayo kuwa yanatokana na masuala ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu.
Katibu wa chama cha maalbino mkoa wa Mwanza, Mashaka Tuju, aliishutumu serikali kwa kushindwa kuchukua hatua stahili tangu mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) yalipoanza miaka tisa iliyopita.
Amesema kwa miaka tisa serikali inahangaika na kudai inachukua hatua lakini hakuna hatua yoyote inayoonekana mpaka sasa huku albino wengi wakiwa wanaishi vijijini katika nyumba zisizo na ulinzi thabiti, lakini utakuta viongozi wa serikali wanaenda huko pale linapotokea tatizo la mauaji ya watu hao.
Tuju amewashambulia mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, Antony Diallo, naibu waziri wa nishati na madini, Charles Kitwanga na mbunge wa Magu, Dk. Festus Limbu, kwa kushindwa kufanya juhudi zozote za kuwalinda na kuwatetea albino.
Katika kipindi cha miezi miwili, watoto Pendo Emmanuel wa Kwimba na Yohana Bahati (mwaka mmoja) wa kijiji cha Ilelema Chato, walitekwa na watu wasiojulikana.

Jumapili, 22 Februari 2015

MKILANIA.COM. Tundu Lissu: Dar es Salaam Mnatutia Kichefuchefu


MKILANIA.COM.Akiwa mgeni mgeni Rasmini katika uzinduzi wa Chaso N.I.T Mbunge wa Singida Mashariki Mh Tundu Lisu Akiongozana na Mbunge wa Ubungo Mweshimwiwa John Mnyika, Amesema haoni haja ya kuyashangilia na kushangilia Matokeo na Ushindi Ambao Ukawa wameupata ktk Matokeo ya Uchaguzi wa Serikari za Mitaa na Vitongoji Vya Jiji la Dar es salaam Kwani CCM imetugalagaza vibaya sana alisema.

Pia Mh Tundu Lisu aliongeza kuwa Katika Historia Nchi zote Zilizofanya Mapinduzi ya Kisiasa Huanzia katika Miji mikuu Na mji kuu wa Tanzania ni Dar es Salaam Dodoma ni danganya Toto Hivyo basi ili MaCCM Yaweze kutoka Madarakani Mh Tundu Lisu Amewataka Wakazi wa Dar es salaam na Vitongoji Vyake Waache Kututia Kichefuchefu ktk Matokeo ya Chaguzi haswa Tunapoelekea ktk Uchaguzi Mkuu Mwezi Octoba, akitolea mifano katika Mikoa ya Kaskazini wakiongozwa na Arusha, Pamoja na Nyanda za juu Kusini wakiongozwa na MBEYA,

Pia aliwataka wakazi wa Dar es salaam Waige mfano wa Jimbo lake Singida mashariki Walivyo wagalagaza MaCCM. Ktk Uziduzi huo Pia Mweshimiwa Tundu Lisu aliwagawia Wanafunzi zaidi ya 120 kadi za CHADEMA. hongeleni sana N.I.T Vyuo vingine viige Mfano Kutoka Kwenu.

Jumamosi, 21 Februari 2015

MKILANIA.COM.Mmiliki wa Clouds Media Group "Joseph Kusaga" akanusha kuiuza Clouds kwa Rostam Aziz


MKILANIA.COM.Baada ya siku ya jana kuzuka uvumi kupitia mitandao ya kijamii kuwa Radio bora Tanzania "CloudsFm" imeuzwa na mmiliki wa kampuni hiyo "Joseph Kusaga" na alieinunua ni mwanasiasa Rostam Aziz.
uvumi huo uliokua unadai kuwa na uhakika kutoka kwa mtu wa ndani na very senior kutoka Clouds Media ulidai kuwa Clouds Media inayomiliki Clouds Fm, Choice Fm na luninga ya Clouds Tv imenunuliwa na tajiri mfanya biashara na mwanasiasa Rostam Aziz.

MKILANIA.COM.Diamond atoa sababu za kushindwa kuhudhuria mazishi ya baba wa Dully Sykes

MKILANIA.COM.Baada ya kutupiwa shutuma na lawama nyingi kupitia mitandao ya kijaa kwa sababu ya kutokuweza kuhudhuria msiba wa marehem baba wa swahiba wake na kaka yake (kama anavyomuita) Dully Sykes, Mzee Abby Sykes huku akionekana akila bata na mpenzi wake Zari zanzibar, Diamond aamua kufunguka upande wake na sababu za kushindwa kufika katika mazishi.
Diamond amesema msiangalie mnachokiona katika Instagram mkajua mtu labda alikuwa anafanya starehe.....


"watu tu waliniona niko zanzibar, lakini ukweli hwajua zanzibar nmeenda kufanya nini, usiangalie kila unachokiona kwenye instagramukajua mtu labda kwasabbu alikuwa anafanya starehe, niko katika kipindi ambacho sio kizuri kwangu mimi, kwangu na kwa familia yangu, kwasababu kuna vitu ambavyo siwezi kuvizungumza, lakini, na siwezi kuweka kwenye media ndio maana watu wengine wanaweza kuniana nacheka nafanya nini, lakini nipo katika situation ambayo, kwanza mama yangu anaumwa sana sijawahi kulizungumza hilo nalizungumza hapa, hapa ninavyoongea na wewe yupo India, so kuna vitu vingi vinaendelea siwezi kusema nilikuwa zanzibar nafanya nini, inawezekana ikawa ndio sababu imenifanya mpaka mimi nikachelewa kwenda kwenye msiba....unajua wakati mwingine ni vizuri kwenda kuzika lakini inawezeka mtu akawa ameenda kuzika lakini mimi nikawa sijaenda kuzika nikawa nimefanya cha maana kuliko alieenda kuzika kwasabau huwezi kujua nimefanya kitu gani.so watu hawakawii kuongea niliskia naambiwa mimi sijui Diamond hajafika lakini naamini watu wengi hawakufika na kila mtu hakufika kwasababu flani.mi sio mpuuzi, kwasababu mimi na Dully ni kama, dully mi ni kama kaka yangu kabisa, ni mtu ambae amenisaidia vitu vingi sana, isingewekana kabisa mi niko na nina nafasi nishindwe kwenda kwenye msiba, ukiacha tu dully lakini mtu aliefariki ni kama mzee wangu na ni mtu ambae amefanya vitu vizuri  amefanya kitu kikubwa katika sanaa hii ya mziki na mi nimefika hapa yeye pia ana mchango wake, so haikuwa rahisi eti mi nisiende tu eti nikiwa sina sababu, kulikuwa sababu na ndio maana." alimaliza kwa kusema Diamond.

MKILANIA.COM.Hongera Millard Ayo:Afungua Kituo cha kurusha mawimbi ya redio

MKILANIA.COM Mtangazaji wako wa nguvu,Millard Ayo mfanyakazi wa Clouds Fm kipindi cha Amplifier amefungua studio kubwa ya kisasa iliyomghalimu mamilioni ya shilingi."Ilikuwa si kazi ndogo kuanzisha hii studio ambayo nimeijenga mwaka mmoja kwa kudunduliza kihasi kidogo kidogo ninachokipata" alisema Millard Ayo.

Ameandika hivi kwenye ukurasa wake wa Facebook:

"Siku zote ni furaha pale ndoto inapokua kweli, nilitamani sana siku moja Millard Ayo kumiliki studio yangu ya Radio kutokana na jasho langu na leo Namshukuru Mungu nimefanikiwa kumaliza ujenzi wa studio yangu baada ya kudunduliza kidogokidogo kwa zaidi ya mwaka mmoja ndio maana hata wewe hutakiwi kukata tamaa kwa chochote hata kama kinachelewa mtu wangu, nilianza kuidizaini hii na baadae watu wangu @francis_ayo na @abdul8819 wa @pixelbasetz wakanisaidia sana yani, nina mengine yanakuja ila kwa leo nimekupa hii tu mtu wangu! hapa panaitwa ‪#‎TZA‬ !! thanks kwa Maboss wangu Joe Kusaga, Ruge na @sebamaganga wamenipa nguvu na nafasi kubwa sana kwenye maisha yangu! birthday yangu ilikua Jan26 na nimejipa hii studio kama zawadi kubwa kwenye maisha yangu baada ya kuihangaikia usiku na mchana bila kukata tamaa"

MKILANIA.COM. Penzi la Wema Sepetu na Ommy Dimpoz, Kumbe Dimpoz ni Boya tu Nyuma ya Pazia kuna Kigogo


MKILANIA.COM. HABARI ya mjini ni kwamba, lile penzi linalonadiwa la Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na mwigizaji Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ limejaa magumashi, ikidaiwa kuwa jamaa huyo kawekwa kama boya tu, nyuma yake kuna kigogo mzito serikalini ndiye anayekula vinono, Risasi Jumamosi limetonywa.


Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Dimpoz ameagizwa na kigogo huyo awe mpenzi kivuli wa Wema ili kuzuga watu wasishtukie mchezo kama yeye ndiye anayesukuma gududumu la malovee kwa Madam.

“Kutokana na unyeti wa kazi yake, jamaa hataki kujitokeza ‘front’ ndiyo maana ameamua kumtumia Dimpoz kama kanyaboya huku yeye akiendelea kula vyake,” kilisema chanzo hicho.Kikizidi kumwaga ubuyu, chanzo hicho kilidai kigogo huyo ndiye anayedhamini safari zote za Wema na Dimpoz nje ya nchi ikiwemo ile ya juzikati nchini Marekani ambayo ilibuma.

“Jamaa ana pesa chafu, amemnunulia Wema viwanja viwili kimoja kipo Tabata na kingine Kigamboni, Dar, ndiye anayemwezesha Wema katika shughuli zake za kila siku.“Kigogo huyo ndiye chanzo cha Wema kummwaga Diamond, alimpotezea kwa sababu ya maslahi zaidi, hata kwenye bethidei ya Wema mwaka jana, kigogo huyo ndiye aliyegharamia vitu kibao hadi kusababisha Diamond ahoji,” kilisema chanzo chetu.

Jitihada za kumsaka kigogo huyo ili azungumzie ishu hiyo hazikuzaa matunda lakini alipotafutwa Dimpoz na kusomewa tuhuma hizo, alijibu:“Watu watambue kuwa uhusiano wangu na Wema upo kwa ajili ya ‘project’ zangu, niacheni please niinjoi maisha yangu kuhusu huyo kigogo muulizeni vizuri Wema mwenyewe,” alisema Dimpoz.

Mwanahabari wetu alipomvutia waya Wema, alijibu kwa kifupi na kukata simu:
“Ujue sasa hivi mimi sitaki malumbano na mtu, najua kila mtu siku hizi anaongea kila anachojisikia, naomba niachwe na maisha yangu, unayoyasema hayana maana,  wanasema kwa sababu hakuna anayemjua mpenzi wangu wa sasa sina muda wa kubishana.”

Hivi karibuni, wakiwa Sauz, Wema na Dimpoz, picha zao wakiwa kimahaba zilivuja mitandaoni hivyo kuibuka gumzo kuwa huenda kwa sasa nao wanatoka.

MKILANIA.COM. Picha Mbali Mbali za Msichana Mwenye Umbo Matata Anayesemekana Kateuliwa Kuwa Mkuu wa Wilaya

MKILANIA.COM.Jana Siku Nzima Msichana huyu anayejulikana kama Nice Chande ama @mwakalicious24 amepaishwa sana kwenye mitandao ikisemekana kuwa Rais kamchangua kuwa Mkuu wa Wilaya ...Watu wengi waliguswa hasa kutokana na umbo lake matata ....Bado hatujapata ukweli wa jambo hili lakini haraka haraka nimeangalia majina ya wakuu wa Wilaya wapya sijaona jina lake labda awe anatumia jina jingine ...Jionee Picha zaidi Hapa Chini:





MKILANIA.COM. Hii ni ya mwanamke kumkata mpwa wake sehemu zake za siri Ruvuma…

knife-blood 
MKILANIA.COM Mtu mmoja wa Kijiji cha Majimaji Ruvuma, Patrick Vitus amekatwa sehemu zake za siri  na kuachwa zikining’inia.
Ofisa Mtendaji Wa Kijiji hicho Hussein Mkali amesema Partick alikatwa sehemu zake za siri na mpwa wake Zainabu Saidi baada ya kumkatalia kwenda kumfuata mume wake anayeitwa Musa Said ambaye alikuwa kwa mke mdogo.
Baada ya kufanya tukio hilo Ofisi ya Kijiji ilimkamata Zainabu na kumpeleka katika kituo cha Polisi, huku Patrick akipelekwa Hospitali ya Tunduru kwa ajili ya matibabu.
Chanzo: Gazeti la Mtanzania, Feb 21 2015.

Alhamisi, 12 Februari 2015

MKILANIA.COM. Kama Ulikuwa Huamini Ushahidi Mwingine wa Wema Sepetu na Ommy Dimpoz Kitandani Huu Hapa


MKILANIA.COM. : Wenzangu na mie ambao mlikuwa hamuamini kuna ka Project kanaendelea kati ya Wema Sepetu na Ommy Dimpoz Basi Hii ni picha nyingine wakiwa Kitandani huku Ommy Dimpoz akiwa kwenye usingizi na Wema Akaibia Selfie huku akitabasamu.......
Je Bado Hujaamini?

MKILANIA.COM.Emmanuel Mbasha: Flora ndiye anayejua ukweli baba wa mtoto aliyejifungua

Akihojiwa na gazeti la Mtanzania baada ya kuahirishwa kwa kesi yake ya ubakaji inayomkabili, amedai kuwa Flora ndiye anayejua ukweli wa nani baba wa mtoto aliyejifungua hivi karibuni.

Ameongea hivyo baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kutokana na kusambazwa kwa picha ya mtoto ikimhusisha kufanana na mchungaji wa kanisa la ufufuo na uzima ndugu Gwajima.

My take: Ukiona mume anasema mke ndiye anayejua ukweli wa nani baba wa mtoto ujue pana walakini juu ya mapenzi yao, anajua alikuwa anachapiwa.

Huyu ndo Kiongozi wa Kikundi cha Kigaidi Kinachoua Polisi na Kuiba Silaha Kwenye Vituo Nchini.....Anaitwa Kaisi Bin Abdullah


MKILANIA.COM.HATIMAYE kuvamiwa kwa vituo vya polisi na kuporwa silaha huku askari wake wakiuawa kikatili kumejulikana kunafanywa na nani kufuatia gazeti hili kunasa mkanda wa video wa mtu mmoja anayejiita Kaisi Bin Abdullah akijitapa kufanya hivyo kwa lengo la kukusanya silaha ili kulipa kisasi siku si nyingi!


Ijumaa liliunasa mkanda huo kutoka kwa mtu mmoja aliyekataa kujitambulisha kwa jina wala kusema anakotokea hapa nchini huku akisema: “Una maneno ya hatari sana, naogopa kujianika, nitauawa.”

Hatimaye kuvamiwa kwa vituo vya polisi na kuporwa silaha huku askari wake wakiuawa kikatili kumejulikana kunafanywa na nani kufuatia gazeti la Ijumaa kunasa mkanda wa video wa mtu mmoja anayejiita Kaisi Bin Abdullah akijitapa kufanya hivyo kwa lengo la kukusanya silaha ili kulipa kisasi siku si nyingi!

Gazeti  hilo linadai  kuunasa  mkanda huo kutoka kwa mtu mmoja aliyekataa kujitambulisha kwa jina wala kusema anakotokea hapa nchini.

Bin Abdullah ametumia dakika 11: 03 kuzungumzia mambo mbalimbali lakini kubwa kuliko yote ni kuliponda Jeshi la Polisi Tanzania kwa kuwakamata wenzao katika imani na harakati (zinazohifadhiwa kwa sasa) na kuwashikilia kwenye mahabusu mbalimbali nchini.

Alianza  kwa  Kusema:
Bin Abullah ambaye kwenye mkanda huo amevaa nguo nyeusi kama ninja na miwani ya giza, alizungumza kwa kirefu, akitoa wito lakini mbele akasema:

Tumeshaungana ili kupambana. Mkoa wa Mtwara zaidi ya wenzetu kumi na saba walikamatwa kwa makosa ya dhuluma, makosa ya kupanga, makosa ya ugaidi.

Ishirini na moja wamekamatwa Zanzibar wako katika Gereza la Segerea (Dar). Wenzetu wengine kumi na nane wamekamatwa Mwanza wako katika Gereza la Kisongo, Arusha. Ndugu zangu, wenzetu wengine kumi na saba wameuawa Mtwara kwa amri ya ...(anamtaja waziri).”

“Subira yetu imefika mwisho na tulichokuwa tunasubiri Mungu ameshatupa. Tunatoa ahadi kilichopo hivi sasa tunatoboa jahazi wote tuzame.

“Tunatoa rai, wenzetu waliopo Gereza la Kisongo waachiwe huru. Hapa hatumtishi mtu yeyote yule.”

“Pili, agizo la Ernest Mangu IGP, umetangaza uliwenguni kwamba umewakamata wote waliovamia vituo vya polisi na umezikamata silaha zote. Ukweli ni kwamba unatetea tumbo lako. Hakuna mtu hata mmoja aliyekamatwa na wala silaha hazijakamatwa.

“Mungu ametukubali. Katika Kituo cha Polisi Ushirombo (Kilimanjaro) tumeweza kuvamia kituo, tukaweza kutoa roho za polisi na tukaweza kuchukua silaha, tunazo.

“Tumevamia Kituo cha Polisi Ikwiriri (Pwani), tumeweza kuchukua silaha za kutosha, tumeweza kuchukua mabomu ya kutosha. Tunazo silaha tunasubiri muda zianze kufanya kazi.

“Ernest Mangu nakupa changamogto, hivi sasa tuna uwezo...(maneno yanahifadhiwa kwa usalama) wakati wowote ambao tunataka.

“Tumeweza kuchukua silaha bila kuwa na silaha yoyote. Ndugu zetu wa Tanga wameweza kuchukua silaha wakiwa hawana silaha yoyote. Ikwiriri tumechukua silaha tukiwa hatuna silaha yoyote, mpaka sasa tumeshachukua roho tano za polisi.

“Ndugu zangu, ...mlikuwa mkinisubiri nitoe tamko, natoa kauli rasmi...” alihitimisha Abdullah, huku vitisho vya jumla kwenye tamko lake vikiwahusu polisi, viongozi wa ngazi za juu serikalini pamoja na mikusanyiko ya ibada.


Tamko  la  IGP
Baada ya video hiyo,Gazeti  la Ijumaa  lilimtafuta  Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu na kuzungumza naye kuhusu mtu huyo na kumkabidhi video ambapo alisema:

“Nawashukuru sana kwa kuleta video hii, huu ndiyo ushirikiano unaotakiwa, nawaomba wananchi video za aina hii wazikatae kwa sababu ni kosa kuwa nazo na watu kadhaa wameshakamatwa kwa kuwa nazo.

“Sisi kama jeshi la polisi tunajua kuwa kuna watu wanadhani kufanya uhalifu kama huo kutawasaidia kutimiza matakwa yao, lakini ukweli ni kwamba polisi wapo imara na nina uhakika watuhumiwa watakamatwa kwa kushirikiana na raia wema.”

Shehe  Mkuu  Amkana
Baada ya kuzungumza na IGP, Gazeti lilimtafuta Shehe Mkuu Tanzania, Mufti Shaban Simba na kumsimulia kuhusu kuibuka kwa Bin Abullah na kutaka kujua pengine anamfahamu.

Kwanza hizo taarifa hizo ndiyo nazisikia kutoka kwako. Hilo jina ulilonitajia (Bin Abdullah) sijawahi kulisikia labda muangalie kwa wenzetu upande wa pili.”

Chanzo:GPL

MKILANIA.COM. Wanaume Masikini na Wasiojiamini Wanaongoza Kutongoza kwa Meseji Nyingi Halafu Ndefu

MKILANIA.COM.Nimekaa sehemu leo napata lunch, mara dada mmoja mrembo aliyekuwa karibu yangu "kareact", "mameseji kibao halafu marefu, hayaeleweki.
Unanijazia tu inbox, utakuwa masikini tu wewe halafu hujiamini".Dah, nilishtuka sana. Baada ya dakika kama 2 hivi..
nikamuuliza dada yangu mbona hasira sana, kwa nini.
Akanijibu "kuna jianaume linanijazia tu inbox, linatuma messages nyingi, ndefu halafu halieleweki, wiki ya pili sasa, mie ananiudhi!"

Nikamwuuliza "mbona unasema atakuwa masikini,akajibu "mtu mwenye hela zake na anayejiamini atahangaika kutuma mameseji kibao, marefu ambayo hata hayaeleweki."

Kwani huyo hawezi kuwa tajiri, lakini kumbe anafanya ufafanuzi kwa kuandika kwa kina,"ingawa simjui, atakuwa hana lolote, anafikiri akijieleza au kuandika sana nitamhurumia au nitamwelewa, akafie mbele huko, tena namblock, hii ni kawaida ya wanaume kapuku."

MKILANAI.COM.Majibu ya Ommy Dimpoz kuhusiana na picha zilizoenea akiwa na Ex wa Diamond Platnumz

.
.
MKILANIA.COM.Miongoni mwa stori zilizochukua headline mitandaoni hata kwenye magazeti ni kuhusu picha ya hitmaker wa ‘Ndangushima’ Ommy Dimpoz akiwa na ex wa Diamond Platnumz ,Wema Sepetu kitandani wamelala pamoja na picha zingine zilizozua mjadala mkubwa.
 Ommy Dimpoz ;Ni picha tu mimi naona kama ni picha zingine tu za kawaida,  sasa nimeshindwa kuelewa kwanini labda zimetengeneza sana stori  kwasababu mimi naona sio mara yangu kwanza kupiga picha na Wema hata uki google utaona tunapicha nyingi sana kwa hiyo sijaelewa kwanini zimeleta stori
May be nafikikiri zilizotengeneza stori zaidi ni hizi ambazo zinaonesha tuko chumbani kwasababu mimi nilikuwa nimelala kiukweli  na tulikuwa tunakaa kwenye apartment moja nilikua nimeshtukia picha zipo kwenye mitandao unajua unavyokaa kwenye apartment kwasababu tulienda kwenye matembezi binafsi na washikaji wengine tulikua wengi wengi kidogo tulienda South Africa unajua mnavyokaa kama familia kunakuwa na mambo ya utani utani nimeshtukia tu picha zimeenea kwahiyo hata watu wakiniuliza ninawambia wamuuliza aliyepiga picha hizo
MKILANIA.COM.; “…Wengi wanafahamu kuwa wewe ni mshikaji wa Diamond Platnumz imekuaje sasa hivi kuonekana kwenye picha na Ex wa Diamond Platnumz,Wema Sepetu…?”
Ommy Dimpoz ; “…Sidhani kama kuna tatizo kwasababu hawa wote ni watu wangu nimefahamia nao siku nyingi nimekuwa nao karibu katika kipindi tofauti kabla hawajakuwa kwenye uhusiano mimi tayari ni watu wangu sidhani mimi nianze kuelezea sijui ooh nilikuwa labda na Wema sehemu, Wema ni mshikaji wangu tangia  siku nyingi kwa hiyo  hata kama alikuwa katika  uhusiano na Diamond yakatokea mahusiano yao pengine hayapo sasa  hivi hayawezi kunifanya mimi kuharibu ushikaji wangu kwasababu hivyo ni vitu vyao  personal“Alisema.
.
.

Jumatano, 11 Februari 2015

MKILANIA.COM. Jionee Jinsi Mkorogo wa Kuchubua Ngozi ulivyomfanya Huyu Mwanaume


MKILANIA.COM. Mwanaume huyu anayeitwa  Pela Tonye Okiemute ni maarufu sana huku Nigeria kwa kazi yake anayoifanya ya kutengeneza Mikorogo ya kujichubua ngozi hasa kwa wanawake , Wenyewe wanamwita "King of Beauty", Wateja wake wakubwa ni Wasanii wakubwa na Wanawake wanaojiita
Socialite kama kina Agness Masogange na Vera Sidika, yeye mwenyewe amejichubua vya kutosha kiasi kwamba kama ulikuwa unamjua zamani kwa sasa uwezi kumtambua , Pale Ameshare picha zake alivyokuwa zamani ujionee jinsi mkorogo ulivyombadilisha:


Despite serious backlash online against skin bleaching and lightening, based on the comments and testimonials on his instagram page @pelsinternational, it is obvious that there is a long list of potential clients who want the same skin results.


Haya Wabongo Mpo ? Kwa wale wanaopenda kujichubua Mtaalam Huyo sasa

MKILANAI.COM. Mfahamu ‘Handsome boy’ wa EPL.

Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud ametajwa kuwa mchezaji mwenye mvuto kuliko wote wanaocheza kwenye ligi ya England katika utafiti uliofanywa miongoni mwa mashabiki hususan wa kike nchini England .
Utafiti huu ulihusisha jumla ya wanawake 250 raia wa Marekani ambao waliulizwa maswali juu ya wachezaji wanaodhani wana mvuto wa kimapenzi nchini England na utafiti huo ulimuonyesha nyota huyu Mfaransa kuwa na mvuto kuliko wote .
Wakati alipoarifiwa juu ya kutwaa tuzo hii isiyo rasmi ya mchezaji mwenye mvuto wa kimapenzi kuliko wote , Olivier Giroud alipewa zawadi ya kioo cha dhahabu na hakusita kuwashukuru wazazi wake wawili kwa kumzaa na kumfanya kuwa na mvuto huu ambao leo umekubalika kuwa bora kuliko wachezaji wote kwenye ligi ya England .
2591873200000578-0-image-a-5_1423658746412
MKILANIA.COM. Giroud pia aliwashukuru watu wengine kama kinyozi wake , mtaalamu wake wa masuala ya make-up, mbunifu wake wa mitindo pamoja na msaidiz wake wa masuala ya picha watu ambao kijumla wanatengeneza timu inayiomfanya aonekane kuwa na mvuto huu alio nao .
Giroud hakuwa mwenyewe kwenye utafiti huu na kuna wachezaji wengine waliotambuliwa kuwa na mvuto akiwemo mchezaji wa Sunderland Santago Vergini ambaye alishika nafasi ya pili  na nyota wa Leicester City Matty James ambaye alishika nafasi ya tatu .

MKILANIA.COM. Chelsea imecheza na Everton nimekuweka matokeo hapa

(null)
MKILANIA.COM. Viongozi wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Chelsea leo ilisafiri mpaka jijini Liverpool kwenda kucheza na vijana wa Roberto Martinez – Everton.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Goodson Park umemalizika kwa Chelsea kuendelea kuimarisha uongozi wao wa pointi 7 baada ya kuifunga Everton 1-0.
Goli pekee la Willian katika dakika ya 89 lilihakikishia Chelsea ushindi muhimu dhidi ya Everton.
Wakati huo huo Manchester City imeifunga Stoke City 4-1. Magoli mawili ya Sergio Aguero na moja Milner na lingine la Samir Nasri likahatimisha ushindi huo wa City ambao wamekuwa na mfululizo wa matokeo mabaya siku za hivi karibuni.
Matokeo ya mechi zote za katikati ya wiki
(null)