MKILANIA.COM. Jeshi la Polisi linawashikilia watu wawili wakazi wa Manispaa ya Tabora kwa tuhuma za kuwanyonga watoto wawili hadi kufa, kisha kuwafukia ndani ya nyumba waliyokuwa wanaishi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Juma Bwire, amethibitisha jana kutokea kwa mauaji hayo ya kikatili na kuwataja watuhumiwa kuwa ni mama mzazi wa watoto hao, Zuhura Masoud (25) na baba yake Shaban Ramadhan (75) wakazi wa Kata ya Chemchem mjini Tabora.
“Baada ya mama huyo kutekeleza
unyama huo, aliwafunga kwa kuwavingirisha kwenye mifuko ya sandarusi
watoto hao Mwamvua Mrisho (4) na mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja
la Sudi kisha kuwafukia chini, mmoja sebuleni na mwingine chumbani
kwake”:-Bwire.
“Tulipata taarifa tukazifanyia kazi
kwa weledi wetu na kubaini ukweli wa mauaji hayo. Huyu mwanamke na baba
yake mzazi mzee Ramadhani tunawashikilia kwa mahojiano zaidi na tunazo
taarifa kwamba walikuwa wakigombea nyumba, inawezekana ugomvi huo labda
ndiyo chanzo halisi cha mama kuamua kuchukua uamuzi mgumu kama huo“:-
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni