Mkilania.com. Timu ya taifa ya Ivory Coast imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika Afcon baada ya kushinda mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Cameroon kwa 1-0.
Bao pekee lililoipa Ivory Coast pointi zote tatu lilifungwa na mshambuliaji Max Alain Gradel ambaye alifunga bao hilo kwenye dakika ya 36 ya mchezo na kuihakikishia timu yake uhakika wa kusonga mbele .
Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Ivory Coast wanafuzu kama washindi wa kwanza wa Kundi D wakiwa wamejikusanyia jumla ya pointi 5 baada ya kutoka sare kwenye michezo miwili na kushinda mchezo mmoja .
Ivory Coast watacheza mchezo wa robo fainali dhidi ya washindi wa pili wa kundi C dhidi ya timu ya taifa ya Algeria huku Ghana wakingoja kumfahamu mshindi wa pili wa kundi D .
Mshindi wa pili wa kundi D atakapatikana hapo kesho (Alhamisi) wakati ambapo itarushwa shilingi kuweza kumpata mshindi kati ya Guinea na Mali ambao wamelingana kwenye rekodi zao .
Mali na Guinea wataamuliwa kwa shilingi baada ya timu hizo kulingana kwenye kila kitu kuanzia pointi , magoli ya kufunga na kufungwa hali itakayolazimu mwamuzi kurusha shilingi kuipata timu itakayokwenda robo fainali .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni