Mkilania.com.Nyota wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Luis Figo ametangaza nia ya kuwania kiti cha urais wa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA katika uchaguzi wa shirikisho hilo utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu .
Figo ametangaza azma hiyo akitumia ukurasa wake binafsi wa mtandao wa kijamii wa Twitter ambapo aliueleza ulimwengu lengo lake la kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho kinachomhusisha rais wa sasa Sepp Blatter .
Figo anakuwa mgombea wa sita kutangaza azma ya kuwania urais wa FIFA baada ya Blatter mwenyewe , mchezaji mwingine wa zamani David Ginola , makamu wa rais wa FIFA
ambaye pia ni rais wa chama cha soka cha Jordan Prince Ali Bin Al
Hussein , rais wa chama cha soka cha Uholanzi Michel Van Praag , na
kiongozi wa zamani wa FIFA Jerome Champagne .
Figo amesema kuwa sababu inayomuongoza
kuingia kwenye mbio hizo ni kuleta mabadiliko ndani ya shirikisho hilo
na kupunguza kashfa zinazoendelea kulikumba shirikisho hilo .
Rais wa sasa wa FIFA Sepp Blatter
anawania nafasi hiyo ikiwa ni mara yake ya tano katika wakati ambao umri
wake umefika miaka 78 .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni