MKILANIA.COM. Kikao cha Bunge kimeendelea leo Dodoma,
wakati wa maswali na majibu moja ya ishu ambayo iliulizwa ni kuhusu
Serikali inafanya jitihada gani kuzuia movie ambazo ziko kinyume na
maadili ya Tanzania.
“Serikali
imeshafanya tafiti zozote zile zinazoonyesha athari ni kwa kiasi gani
utamaduni wetu umeathirika? kwa kuwa kasi ya utandawazi ni kubwa sana
sana na kasi ya Serikali kuwisha au kuimarisha hizo sera na sheria ni
ndogo sana,na kundi linaloathirika ni vijana,Serikali haioni kasi hiyo
ndogo waliyonayo itaangamiza nguvu kazi ya Taifa na kupoteza tamaduni
zetu zote?”– Mbunge Amina Mwidau.
Akijibu kuhusu suala hilo Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Nkamia amesema; “Serikali
kwa upande wake tuna vyombo mbalimbali vinavyosimamia jambo hili,kwanza
ni bodi ya filamu ambayo husimamia filamu zinazotoka nje na ndani ya
nchi,ili kuhakikisha zinazoingia kwenye soko zinafata maadili,tuna
Baraza la Kiswahili la Taifa BAKITA kazi yake ni kuhakikisha lugha iko sawa, lakini pia tuna kamati ta maudhui ipo chini ya TCRA kazi yake ni kusimamia maudhui“
Baada ya majibu hayo Mbunge Maryam Msabaha aliuliza; “Wasanii
wengi wanaiga mambo ya kimagharibi na filamu zao nyingi wanazozionyesha
zinakiuka maadili ya Mtanzania, Je Serikali inachukua hatua gani
kuzuia filamu hizo?”
“Hakuna
filamu inayoingia sokoni bila kutizamwa na kuruhusiw na bodi ya filamu
na inahakikisha haiharibu utamaduni wa mtanzania,tunajua zipo
zinazoingia kwa njia ya panya lakini kuna njia ambazo tunatumia
kuwakamata, zipo filamu nyingine zimeteketezwa kutokana na kutoridhika
nazo“– Juma Nkamia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni