Tafuta katika Blogu Hii

Jumanne, 3 Februari 2015

Kutoka #MkasiTV, haya ni TISA kwa sauti yake BEN POL niliyokuwekea hapa…

Mkasi IISaa chache zilizopita kwenye show ya mkasi staa wa R&B Tanzania, Ben Pol alikuwa kwenye interview, safari yake kwenye muziki, ishu ya bangi, ni baadhi ya alivyozungumzia.
Safari yake ilianzia kuimba RAP kabla ya R&B; “Form three makundi ya washkaji wakaniambia unaweza ukajaribu kuimba, una sauti nzuri.. nikawa naiga nyimbo za TID, Banana… Nikawa napenda muziki lakini sijui exactly nataka nini kwenye muziki
Nikaenda THT, nikaambiwa imba nikaanza kuimba… nikatoa sauti wakasema lakini ana tone nzuri, nikapata zali nikaambiwa ingia darasani… Nikaanza na mimi kufundishwa, nikawa na-improve
Kuhusiana na malalamiko ya baadhi ya wasanii wa THT kwamba hawapewi nafasi za kutoka, Ben amesema “Unapokuwa chini ya management fulani, lazima uwe na ile management na lazima kuwe kuna wewe… lazima ubakie na kitu chako kwamba mimi nataka nini…
Collabo yake na Nikki Mbishi kwenye ‘Playboy’ Ben alienda studio kwa Duke akiwa amemsindikiza mwenzake; “muda huo Nikki Mbishi anarekodi ndani Playboy, Duke akakumbuka kwamba ‘huyu si alishawahi kuja kurekodi hapa nyimbo ya kuimba imba hapa.. hebu ingia ndani.. Katika kitu ambacho kichwani kwangu nilikuwa natembea nacho nikasema nikikutana na mtu ambaye yupo kwenye nafasi nzuri akiniambia imba, namkomesha hatoki…Mkasi IV
Ishu ya kutumia bangi je? “Pale kwenye maisha ya form five na six niliwahi kujaribu, sasa hivi situmii kilevi chochote.. sivuti sinywi…
Muziki naupenda, kama kitu hakijatokea vizuri, mi’ pia inaniuma. Nilifanya show moja Dodoma, nilifika pale tukaanza kupiga acapella karibia dakika kumi nzima uwanja unaimba.. nilivyokuja kuweka CD ndio nikaharibu show mpaka watu huku chini wakaniambia Ben ulitakiwa uishie palepale kwenye acapella…
Mkasi III
Kuhusu Grace Matata kutofanya vizuri kwa sasa; “ Niongee kama shabiki na mtu ambaye nimewahi kufanya naye kazi kwenye lebo moja.. nilivyoingia kwenye ile lebo niliwakuta wasanii wakiwa wana kama miaka miwili hivi akiwemo Grace. Hakukuwa na mtu amekamilisha album.. in three months nna album iliyoshiba ya nyimbo kumi ndani ya mwaka tuzo.. tour.. Ben Pol yuko kila sehemu. Hapo kuna mwenyezi MUNGU halafu kuna bidii nahisi…”– Ben Pol.
Ya wake ya moyoni kuhusu skendo za mastaa; “ Skendo ambayo ni ya ukweli mi sina noma nae, ya kutengeneza ya kuzidisha ile ndo naonaga miyeyusho… naona kama siku unaweza ukachokwa
List ya wasanii ambao wanamchekesha na anaenjoy kuwa nao ni hii; “Barnaba, Baba Levo, AT ndo namba moja. Kama mnasafiri unaenjoy safari nzima…
Mkasi V
Mkasi VI

Hakuna maoni: