MKILANIA.COM. Ni siku nyingine ngumu kwa Raisi wa FC Barcelona Josep Maria Bartomeu.
Huku uchaguzi mkuu ukiwa umekaribia ndani ya Nou Camp, nafasi ya Bartomeu kurejea madarakani imeingia shakani leo jumanne baada ya kutoka kwa tuhuma zinazomhusisha raisi huyo wa sasa na mambo ya kukwepa kodi.
Sakata hilo la kukwepa kodi linahusisha kesi ya usajili wa Neymar kutoka Santos mwaka 2013.
Kwa muda mrefu kumekuwepo na utata juu fedha iliyolipwa kwenye usajili wa Neymar na Barcelona – mwendesha mashtaka wa kesi dhidi ya Barca anadai Barca waliwalipa Santos kiasi cha €94.8m kwa jumla (€82.7m za ada ya usajili huku €12.1m za kodi), wakati Barcelona wakisema walilipa kiasi cha €57.1m tu.
Bartomeu, pamoja na rasi aliyejiuzulu Sandro Rosell, wanatuhumiwa kwa kupika taarifa za uongo katika uhamisho huo wa Neymar – na matokeo yake Bartomeu anashatakiwa kwa kuhusika na kukwepa inayofikia kiasi cha €2.8m.
Bartomeu anatarajiwa kwenda mahakamani baadae mwaka huu kujitetea dhidi ya mashtaka haya, kwa pamoja na raisi aliyejiuzulu mwezi uliopita kutokana na tuhuma hizo Sandro Rosell.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni