Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 6 Februari 2015

MKILANIA.COM. Wiz Khalifa analetewa drama na baby mama wake Amber Rose??????


 
 
MKIANIA.COM. Ndoa ya wizi Khalifa na Amber Rose ilishafika mwisho na kupeana talaka, lakini tofauti na mastaa wengi, mambo yao wameyaweka kibindoni na kutokuyaongelea hadharani.

 
 
Lakini inaonekana kwa sasa uhusiano wao kama wazazi unaonekana kushindwa kuelewana kwasababu Wiz Khalifa ameingia mtandao wa twitter na kuongea juu ya story kuwa hatengi muda wa kutumia na mtoto wake.

MKILANIA.COM. Picha za Raisi Mugabe akianguka zavuruga mitandao ya kijamii


MKILANIA.COM.  Raisi wa Zimbabwe Robert Mugabe, 90, alianguka mpaka chini mara tu baada ya kumaliza speech aliyokuwa akiitoa kwa wafuasi wake waliokuja kumpokea airport  baada ya safari yake kutoka Ethipia, ijumaa iliyopita.

Mugabe ameanguka baada ya kukosea ngazi alipokuwa akishuka tayari kwa kuingia kwenye gari lake.

Baada ya picha hizo kusambaa, maraia wakaanza kazi yao ya kutengeneza memes zilizozagaa katika mitandao ya kijamii. hizi ni baadhi tu ya picha hizo






MKILANIA.COM. Adhabu walizopewa Morris na Nyosso kwa vitendo walivyowafanyia Okwi na Maguri

Screen Shot 2015-02-06 at 2.29.30 PMMKILANIA.COM. Wiki mbili zilizopita katika mechi za ligi kuu kulitokea matukio mawili ambayo yalileta mjadala mkubwa miongoni mwa wadau wa soka nchini.
Mchezaji wa Azam FC Aggrey Morris alipiga kiwiko Emmanuel Okwi katika mechi iliyowakutanisha Simba vs Mtibwa – kitendo ambacho kilipelekea Okwi kuzimia uwanjani na kupelekwa hospitali – kitendo kingine kilikuwa kikimhusisha mchezaji wa Mbeya City Juma Nyosso ambaye alionekana akimshika makalio mchezaji wa Simba Elias Maguri.
Baada ya mjadala mkubwa kwenye magazeti na mitandaoni hatimaye leo hii Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imewafungia kati ya mechi tatu na nane wachezaji Juma Nyoso wa Mbeya City
na Aggrey Morris wa Azam kutokana na makosa ya kinidhamu waliyoyafanya
wakiwa uwanjani.
Nyoso ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumfanyia vitendo vya udhalilishaji
mshambuliaji Elias Maguri wa Simba amefungiwa mechi nane za Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL). Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Ibara ya 57 na Ibara ya
11 (f) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.
Akiwa mbele ya Kamati hiyo jana (Februari 5 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam, Nyoso alikiri kufanya na kujutia kosa hilo, pia amemuomba radhi
mchezaji Maguri kwa kitendo hicho.
Akisoma uamuzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Jerome Msemwa
alisema kitendo kilichofanywa na Nyoso ni kosa kubwa, kudhalilisha utu wa
mtu, na ni mfano mbaya kwa watoto na jamii nzima ya mpira wa miguu.
Naye Morris amefungiwa mechi tatu za VPL baada ya kutiwa hatiani kwa
kumpiga mshambuliaji Emmanuel Okwi wakati timu hizo zilipopambana kwenye
mechi ya ligi iliyochezwa Januari 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kabla ya kusoma uamuzi, Wakili Msemwa alisema mlalamikiwa Morris alikiri
kugongana na Okwi, kwa maelezo kuwa aliingia kwenye ‘reli’ ndiyo ukatokea
mgongano huo.
Kamati baada ya kupitia malalamiko ya klabu ya Simba, ripoti za Brain CT
scan kutoka Besta Diagnostic Centre na nyingine kutoka Taasisi ya Mifupa
Muhimbili (MOI), taarifa za madaktari zilionyesha Okwi aligongwa kichwani
akiwa anacheza mpira na kuzimia kwa dakika tano, pia mkanda wa video
uliowasilishwa na TFF imeona kulikuwa na kugongana kati ya wachezaji hao.
Hivyo, Kamati ikamtia hatiani Morris kwa kutumia Ibara ya 48(1)(d) ya
Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012 kwa kumfungia mechi hizo tatu na
kumpa onyo kali.

Maskini ile Ofisi ya Kanumba the Great Films Yafungwa Rasmi, Mama na Wadogo zake Kanumba Washindwa Kuiendesha

MKILANIA.COM. : Kuna Msemo unasema Asiyekuwepo na lake halipo , Wengi tunamkumbuka Mwigizaji Marehemu Kanumba alivyobadili mchezo wa Bongo Movies Mpaka kuwa ni Tasnia yenye kukimbiliwa na Wengi ....Sasa Habari tulizozipata ni
kuwa ile Ofisi yake aliyoiacha baada ya Kufariki Dunia Mama Kanumba na Wadogo zake Walio Ahidi kuiendeleza Wameshindwa na Wameamua Kuifunga baada ya Kukosa Kodi ya kulipia Jengo ...Mama Kanumba amekaririwa akisema kwa sasa Kodi ni laki sita hela ambayo wameshindwa kuilipa kwani Kanumba aliacha Kodi ilikuwa Laki Mbili.

Toka Kanumba Afariki Ofisi hiyo iliweza kutoa Filamu mbili tu na Ambazo Hazikufanya Vizuri sana Katika Soko..

Picha ya Mahaba ya Wema Sepetu na Ommy Dimpoz Yazua Jambo, Mashabiki Wamtaka Aanzishe Project na Dimpoz Kumsahau Diamond

MKILANIA.COM: Baada ya Picha ya Wema Sepetu na Ommy Dimpoz Kuwekwa Mtandaoni ikionyesha wawili hao kukaa mkao wa kimahaba huku wema Sepetu Akimtumbua Ommy Dimpoz Chunusi Usoni ..Washabiki mbali mbali wa Wema Wamesifia Picha Hiyo na Kusema.........
Wamependezwa na Wawili Hao Wanavyopendeza na Kuwataka waanzishe Project Mpya , wakiwa na maana wawe wapenzi , Mashabiki wengine walikwenda mbali zaidi na kumwambia Wema Atoke na Ommy Dimpoz ili Amsahau aliyekuwa Mpenzi wake wa Zamani Diamond Platnumz ambae kwa sasa anatoka na Zari the lady Boss wa Uganda..

Baadhi ya Comments za Mashabiki Kutoka Instagram hizi Hapa:

husna1112
pendeza sana my wema huyu ndo mwanaume anaga makuu yuko humble sana

theresiasebastiane
Gooooooooooooooaaaaaaaaaaaaaal hapana refa kaotea dimpoz unataka ufunike 2015 tulia na huyo ndo mwanamke bright na katulia yaani umeokota dodo kwenye mti wa ubuyu pyeeeeeeee refa anzisha mpira ligi imefika patamu

schollah24
Mewapenda b ureeeeeeeeeeeeeeeee @ommydimpoz @wemasepetu

vquetamari
Kwa mfanooooo  ikawa kaukwel??

Je Unaona Wanaendana?

MKILANIA.COM. Hussein Machozi Anaswa na Mchepuko wa Kidhungu, ni Baada ya Kumtelekeza Mke Wake wa Kimombasa


MKILANIA.COM.: Kama ulikuwa unajiuliza Hussen Machozi Yupo wapi baada ya kupotea kwenye Ramani ya Muziki basi leo utapata jibu hapa.
Hivi Karibuni Mwanamke mmoja wa Kimombasa alisikika kwenye vyombo vya Habari na kusema walifunga ndoa na Hussein machozi kwa Siri na baada ya ndoa Hussein Machozi Akamtelekeza ..Sasa habari mpya ni kuwa Hussein Machozi Ametulia kimapenzi kwa Mzungu kwa sasa na Ameshikiliwa Kinoma kiasi cha kwamba afurukuti kwa mzungu huyo..na labda ndio sababu ya kimya chake katika Muziki..

Embu Mshauri Hussen Machozi Chochote
.

Picha ya Nay wa Mitego Akiwa na Msichana Uchi Kitandani Yazua Mjadala, Wengi Wasema ni Udhalilishaji wa Mwanamke


MKILANIA.COM. Picha hii imepostiwa kupitia Account ya msanii wa Nay Wamitego ya Instagram akiwa yupo kitandani na mwanadada ambae amevalia bikini huku sehemu kubwa ya mwili wake ukiwa wazi unaonekana.
Hali ya mwanadada huyo ameonekana akitabasamu bila kuwa na wasi wasi kitendo ambacho kinafanya tuamini kwamba labda wana shoot video, lakini sidhani kama ni sawa pia kwa maadili yetu ya Kitanzania.

Pengine si vibaya lakini mazoea hayo kwetu Watanzania ni mageni.
Picha hii imeonekana kuchukiza mabinti wengi na kuenea kwa story tofauti kwa muda mfupi tangu aipost.

Je Una maoni Gani?

Msanii wa Bongo Movies Akiri Kufanya Biashara ya Kubeba Unga na Kuwauza Wasichana Wenzake kwa Wanaume


MKILANIA.COM.: Akihojiwa na Mtandao wa GPL Msanii Lungi Ameulizwa Maswali Mbali mbali , ambayo yamenishtua kidogo ni haya mawili hapa chini ambayo amekiri yote kuwahi kuhusika nayo

mkilania.com: Wafanyabiashara wengi hasa wanaokwenda nchi hizo ulizotaja wanadaiwa kufanya biashara ya ‘sembe’. Wewe ushawahi kubeba mzigo?

Lungi: Ukweli nimewahi kubeba unga na kuwa mfanyabiashara mzuri tu lakini nimeacha kwani niligundua ni biashara mbaya sana na naomba Mungu anisamehe.

mkilania.com: Unatajwa kuwa mmoja wa mastaa wenye tabia ya kuwaunganisha wenzako kwa wanaume, hili nalo likoje?

Lungi: Ilikuwa zamani lakini sasa nimeacha, nimeona ni kazi isiyo na manufaa kwangu.

MKILANIA.COM. Irene Uwoya wa Bongo Movies Ajiachia Kihasara Dunia Nzima Ishuhudie Upaja Wake wa Kuvutia..Jionee Hapa


MKILANIA.COM: Hivi Jamani ni kweli msanii ili uendelee kuwa midomoni kwa watu kila mara lazima uwe na Skendoz ama kuweka picha za Kiasara Mitandaoni? Haya kwa wale mafisi huo ndo upaja wa Mwigizaji Irene Uwoya ......Meseji Imefika...

Kazi Ipo Bongo Movies....

MKILANIA.COM. Muswada wa Mahakama ya Kadhi Waondolewa Bungeni



MKILANIA.COM. Muswada wa Sheria ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara hautajadiliwa katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma baada ya serikali kuuondoa kwa maandalizi zaidi.



Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, alisema jana usiku kuwa wameamua kuuondoa muswada huo ili kupata fursa ya kutoa elimu zaidi kwa viongozi wa dini na kuufanyia marekebisho baadhi ya maeneo.

Alisema serikali inatarajia kuurejesha tena bungeni mwezi ujao. Hata hivyo, habari za uhakika kutoka Dodoma zinasema kuwa kulikuwa na mvutano mkali ndani ya kamati ya Bunge iliyokuwa inashughulikia muswada huo uliokuwa kwa misingi ya imani hivyo busara ilitumika kuahirishwa uwasilishwaji kwa mara ya pili kwani mjadala kwenye Bunge zima ungeweza kuleta mpasuko.

Muswada huo ulikuwa unawasilishwa kutokana na ahadi ya serikali kwenye Bunge Maalum la Katiba ambako mjadala ulikuwa mzito baadhi ya wajumbe wakitaka mahakama ya kadhi iingizwe kwenye Katiba Inayopendekezwa, lakini Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akashauri kutungwa kwa sheria ya mahakama hiyo, badala ya kuuingiza kwenye katiba.

Tangu serikali itangaze kuwa itawasilisha muswada huo bungeni, kumekuwa na mvutano ndani ya jamii, kundi moja likiupinga kwa madai kuwa serikali haipaswi kujihusisha na masuala ya dini kama katiba inavyoelekeza. Ilielezwa kwamba kama Waislamu wanahitaji mahakama hiyo, basi waunde kwa njia zao wenyewe bila kuhusisha serikali.

Hata hivyo, serikali ilisema kuwa imeandaa muswada huo ili kuweka utaratibu wa kuundwa kwa mahakama hizo kisheria, lakini suala la uendeshaji wake na gharama hazitabebwa na serikali bali Waislamu wenyewe.

Tayari jumuiya za Kikristo kupitia maaskofu wao wamekwisha kutoa msimamo wao juu ya mahakama hizo wakisema kuwa siyo jukumu la serikali kuzianzishwa

Jumatano, 4 Februari 2015

MKILANAI.CO. Moja ya story za mitandaoni, ni hii ya dalili za mgogoro wa Jay Z na Beyonce

NBA All-Star Game 2013 
Mara nyingi mastaa hawa Beyonce na Jay Z wamekuwa ni watu wa furaha na wakati wote huwa pamoja lakini ni mara chache kwa wawili hawa kuwakuta wakiwa wanagombana katika sehemu yenye mkusanyiko wa watu.
bey argung
Beyonce akizozana na Jay Z wakati wakipata chakula
Wakiwa ndani ya mgahawa wa Sushi iliopo Los Angeles wakipata chakula walionekana kutofautiana huku Beyonce akionekana kukasirika na kuwa mkali baada ya kuanzisha ugomvi huo dhidi ya mumewe.

Kilichojadiliwa leo Bungeni kuhusu Movie zinazoingia sokoni Bongo kiko hapa…

Ray
MKILANIA.COM. Kikao cha Bunge kimeendelea leo Dodoma, wakati wa maswali na majibu moja ya ishu ambayo iliulizwa ni kuhusu Serikali inafanya jitihada gani kuzuia movie ambazo ziko kinyume na maadili ya Tanzania.
Serikali imeshafanya tafiti zozote zile zinazoonyesha athari ni kwa kiasi gani utamaduni wetu umeathirika? kwa kuwa kasi ya utandawazi ni kubwa sana sana na kasi ya Serikali kuwisha au kuimarisha hizo sera na sheria ni ndogo sana,na kundi linaloathirika ni vijana,Serikali haioni kasi hiyo ndogo waliyonayo itaangamiza nguvu kazi ya Taifa na kupoteza tamaduni zetu zote?”– Mbunge Amina Mwidau.
Akijibu kuhusu suala hilo Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na  Michezo Juma Nkamia amesema; “Serikali kwa upande wake tuna vyombo mbalimbali vinavyosimamia jambo hili,kwanza ni bodi ya filamu ambayo husimamia filamu zinazotoka nje na ndani ya nchi,ili kuhakikisha zinazoingia kwenye soko zinafata maadili,tuna Baraza la Kiswahili la Taifa BAKITA kazi yake ni kuhakikisha lugha iko sawa, lakini pia tuna kamati ta maudhui ipo chini ya TCRA  kazi yake ni kusimamia maudhui
Baada ya majibu hayo Mbunge Maryam Msabaha aliuliza; “Wasanii wengi wanaiga mambo ya kimagharibi na filamu zao nyingi wanazozionyesha  zinakiuka maadili ya Mtanzania, Je Serikali inachukua hatua gani kuzuia filamu hizo?”
Hakuna filamu inayoingia sokoni bila kutizamwa na kuruhusiw na bodi ya filamu na inahakikisha haiharibu utamaduni wa mtanzania,tunajua zipo zinazoingia kwa njia ya panya lakini kuna njia ambazo tunatumia kuwakamata, zipo  filamu  nyingine zimeteketezwa kutokana na kutoridhika nazo“– Juma Nkamia.

MKILANIA.COM. Rais Kikwete Afichua SIRI Kipigo cha Lipumba.....Asema sheria za nchi lazima Zifuatwe


MKILANIA.COM
SIKU chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na wafuasi wake kupigwa na polisi, Rais Jakaya Kikwete amesema tukio hilo limetokea kwa sababu
nchi inaongozwa kwa sheria na atakayekiuka atakumbana na mkono wa sheria.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya mazungumzo ya faragha na mgeni wake, Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck, ambaye yuko nchini kwa ziara ya siku tano.

Kabla ya Rais Kikwete kutoa kauli hiyo, Rais Gauck aliimwagia sifa Tanzania kutokana na namna inavyofuata utawala wa sheria, uhuru wa vyombo vya habari na kulinda haki za binadamu.

Baada ya viongozi hao kuzungumza mbele ya waandishi wa habari juu ya ziara hiyo, waandishi walipewa fursa ya kuuliza maswali na ndipo mmoja wa wanahabari kutoka Ujerumani, alipotaka kauli ya Rais Kikwete na Rais Gauck, juu ya msingi wa uhuru wa vyombo vya habari na haki za binadamu nchini, wakati hivi karibuni gazeti la The East African lilifungiwa na wanachama wa CUF kupigwa na polisi walipotaka kuandamana.

Akijibu swali hilo, Rais Kikwete alisema: “Tuna sheria zinazoongoza mambo hayo, huwezi kuamka tu ukaamua kuandamana, tuna taratibu zetu za vyama vya siasa kukusanyika, wala hatubani haki na uhuru wa wapinzani, ukivunja sheria hiyo utawajibishwa.

“Na hapa wapinzani ndio wanafanya mikutano mingi kuliko chama tawala, ikitokea hawajafuata taratibu, hatuwezi kuwaacha waendelee kuvunja sheria,” alisema Rais Kikwete.

Jumanne, 3 Februari 2015

MKILANIA.COM. Jingine kubwa kutoka kwenye kesi ya kukwepa kodi kwenye usajili wa Neymar

073014-Soccer-FC-Barcelonas-Brazilian-Neymar-J2-PI.vadapt.620.high.0






 MKILANIA.COM. Ni siku nyingine ngumu kwa Raisi wa FC Barcelona Josep Maria Bartomeu.
Huku uchaguzi mkuu ukiwa umekaribia ndani ya Nou Camp, nafasi ya Bartomeu kurejea madarakani imeingia shakani leo jumanne baada ya kutoka kwa tuhuma zinazomhusisha raisi huyo wa sasa na mambo ya kukwepa kodi.
Sakata hilo la kukwepa kodi linahusisha kesi ya usajili wa Neymar kutoka Santos mwaka 2013.
Kwa muda mrefu kumekuwepo na utata juu fedha iliyolipwa kwenye usajili wa Neymar na Barcelona – mwendesha mashtaka wa kesi dhidi ya Barca anadai Barca waliwalipa Santos kiasi cha €94.8m kwa jumla (€82.7m za ada ya usajili huku €12.1m za kodi), wakati Barcelona wakisema walilipa kiasi cha €57.1m tu.
Screen-Shot-2015-02-03-at-11.16.57-AM
Bartomeu, pamoja na rasi aliyejiuzulu Sandro Rosell, wanatuhumiwa kwa kupika taarifa za uongo katika uhamisho huo wa Neymar – na matokeo yake Bartomeu anashatakiwa kwa kuhusika na kukwepa inayofikia kiasi cha €2.8m.
Bartomeu anatarajiwa kwenda mahakamani baadae mwaka huu kujitetea dhidi ya mashtaka haya, kwa pamoja na raisi aliyejiuzulu mwezi uliopita kutokana na tuhuma hizo Sandro Rosell.

MKILANIA.COM. Diamond Ampeleka Mpenzi Wake Zari Songea..Watua na Ndege ya Kukodi


MKILANIA.COM. Kama ni Kufika basi kwa Zari Diamond Amefika Mwisho wa Reli Kigoma, Toka mapenzi yaanza Diamond na Huyu Mrembo imekuwa tofauti kidogo na wapenzi wake wa nyuma..ambao alikuwa haongozani nao.....



 kwenye Show zake ila huyu wa sasa ni mguu kwa mguu....

Hapa kwenye picha wakiwa uwanja wa ndege wa Songea ....

MKILANIA.COM. Mdada Aliyekwambia Kujua Kuzungusha Kiuno ndo Tiketi ya Kupata Ndoa Kakudanganya..


MKILANIA.COM. Kila mwanamke anavitu vyake alivyojiwekea, ambavyo anataka mwanaume wa ndoto zake awe navyo. Ikitokea akampata Mwenye hivyo vitu basi huona kamaliza kila kitu, anajisahau, anafurahia vile anavyoviona kwa nje na kitandani, badala aanze kumsoma huyo Mwanaume. Kama ni husband material....



Wanawake ndio wanaongoza kwa kulizwa Sana kwenye mahusiano kuliko wanaume, kwasababu mwanamke akishampata mwanaume aliyekuwa anamtaka basi atampenda kwa kila kitu, moyo na mwili wake wote kwa haraka wakati yeye mwanaume hakupi vyote anakuangalia kwanza mpaka atakapoona kweli ndio kitu anachokitaka ndio ataanza kukupenda kwa ukweli sasa. Lakini akiona hakuna kitu atakuchukulia poa poa na baadaye anakupotezea, sasa wewe uliyekufa na kuoza lazima upate ugonjwa wa moyo.

Mwanamke usiende kwenye mahusiano kwa kuangalia picha ya nje, anza kwanza kumwangalia Kama anaweza kuwa Mume na je unampenda kweli, ukijihakikishia hapo anza kuwa wife material msaidie mwanaume hata kwa mawazo tu sio unakaa tu kazi yako wewe ni kuzungusha kiuno tu.

Inatakiwa ukiingia kwenye maisha ya mwanaume mwenyewe anakiri hakuna mwanamke Kama wewe. Unambadilisha hata Kama hakuwa muoaji ajue umuhimu wa mke na kutaka kukuoa.

MKILANIA.CO. Mrembo Tiara Kutoka Kenya Atoa Meseji za Siri Anazochat na Diamond..Zisome Hapa

MKILANIA.COM.Demu wa Kenya anayejulikana kama TIARA ametutumia meseji akidai kwa sasa mambo yake na Diamond ni Safi kwani wanachat Facebook kwa siri ..Soma meseji hizo Hapa chini:







Mdau Je Kweli Huyo anaechat nae ni Diamond ?

MKILANIA.COM. Siri Imefichuka, Mimba ya Aunty Ezekiel Sio ya Moze Iyobo Kama Wengi Wanavyodhani



MKILANIA.COM. Wakati tetesi zikizagaa kila kona ya mji , kuhusu ujauzito wa star wa movie ya 'Young Billionaire', Aunty Ezekiel kuwa amenasa ujauzito wa dancer wa mwanamuziki maarufu nchini, Diamond Platnums aitwaye Moze Iyobo. Licha ya dancer huyo kuinadi mimba ya mpenzi wake huyo mitandaoni , Aunty ameibuka na kudai ujauzito alionao sio wa dancer huyo....
kama watu wanavyojua bali ni ya mtu mwingine ambaye kwa mujibu wa Aunty amesema atajulikana soon baada ya kichanga hiko kilichopo tumboni kuzaliwa.

Paparazi: Mambo vipi? Kwema lakini Aunt? Ehne leta maneno, mna mipango gani na baba mtoto mtarajiwa, Iyobo?

Aunt:Hahaha mimi mzima! Kuhusu Iyobo, mh! Kanipa mimba! Si kweli, nitakapojifungua nitamtaja baba wa mtoto wangu.

Paparazi: Mbona Iyobo amekuwa akijinadi kwenye vyombo vya habari kuwa mzigo ulionao ni wake?

Aunt: Mh! Jibu langu ni hilo nililokupa.

Kajala:Acheni Akili za Kijinga Mavazi yangu Haya Haribu Tabia ya Mtoto Wangu, Kama Ataaribika kwa Kuniona Nimevaa Tumbo Wazi Basi ni Mbumbu

MKILANIA.COM.-Kajala ameshindwa Kujizuia na kuamua kuwashukia wale wote wanaosema anamwaribu mtoto wake kwa Mavazi anayovaa...Soma alichoandika hapa chini:



"Naomba niwaulize binadamu alie kwambia mimi nikivaa hivi nitamuhalibu mtoto nani ? acheni akili za kijinga kwasababu wengi wetu tunajua kabisa mtoto hawi na tabia mbaya kwasababu anamuona mama yake kavaa dira au tumbo wazi sisi zamani wazazi wetu walikuwa wanavaa hivi lakini mbona tuliwasumbua mnaboa na kukera pia kama mtoto wangu atahalibika kisa kaniona mimi nimevaa tumbo wazi utakuwa ni umbumbu wake na ujinga wake lakini sidhani kama mavazi yanamualibu mtoto naisi nimalezi peke yake kama nakuboa usipite hapa tafadhali".

Kajala aliandika na kutupia picha hiyo juu mtandaoni.

Je Wewe Unamaoni Gani?

Kutoka #MkasiTV, haya ni TISA kwa sauti yake BEN POL niliyokuwekea hapa…

Mkasi IISaa chache zilizopita kwenye show ya mkasi staa wa R&B Tanzania, Ben Pol alikuwa kwenye interview, safari yake kwenye muziki, ishu ya bangi, ni baadhi ya alivyozungumzia.
Safari yake ilianzia kuimba RAP kabla ya R&B; “Form three makundi ya washkaji wakaniambia unaweza ukajaribu kuimba, una sauti nzuri.. nikawa naiga nyimbo za TID, Banana… Nikawa napenda muziki lakini sijui exactly nataka nini kwenye muziki
Nikaenda THT, nikaambiwa imba nikaanza kuimba… nikatoa sauti wakasema lakini ana tone nzuri, nikapata zali nikaambiwa ingia darasani… Nikaanza na mimi kufundishwa, nikawa na-improve
Kuhusiana na malalamiko ya baadhi ya wasanii wa THT kwamba hawapewi nafasi za kutoka, Ben amesema “Unapokuwa chini ya management fulani, lazima uwe na ile management na lazima kuwe kuna wewe… lazima ubakie na kitu chako kwamba mimi nataka nini…
Collabo yake na Nikki Mbishi kwenye ‘Playboy’ Ben alienda studio kwa Duke akiwa amemsindikiza mwenzake; “muda huo Nikki Mbishi anarekodi ndani Playboy, Duke akakumbuka kwamba ‘huyu si alishawahi kuja kurekodi hapa nyimbo ya kuimba imba hapa.. hebu ingia ndani.. Katika kitu ambacho kichwani kwangu nilikuwa natembea nacho nikasema nikikutana na mtu ambaye yupo kwenye nafasi nzuri akiniambia imba, namkomesha hatoki…Mkasi IV
Ishu ya kutumia bangi je? “Pale kwenye maisha ya form five na six niliwahi kujaribu, sasa hivi situmii kilevi chochote.. sivuti sinywi…
Muziki naupenda, kama kitu hakijatokea vizuri, mi’ pia inaniuma. Nilifanya show moja Dodoma, nilifika pale tukaanza kupiga acapella karibia dakika kumi nzima uwanja unaimba.. nilivyokuja kuweka CD ndio nikaharibu show mpaka watu huku chini wakaniambia Ben ulitakiwa uishie palepale kwenye acapella…
Mkasi III
Kuhusu Grace Matata kutofanya vizuri kwa sasa; “ Niongee kama shabiki na mtu ambaye nimewahi kufanya naye kazi kwenye lebo moja.. nilivyoingia kwenye ile lebo niliwakuta wasanii wakiwa wana kama miaka miwili hivi akiwemo Grace. Hakukuwa na mtu amekamilisha album.. in three months nna album iliyoshiba ya nyimbo kumi ndani ya mwaka tuzo.. tour.. Ben Pol yuko kila sehemu. Hapo kuna mwenyezi MUNGU halafu kuna bidii nahisi…”– Ben Pol.
Ya wake ya moyoni kuhusu skendo za mastaa; “ Skendo ambayo ni ya ukweli mi sina noma nae, ya kutengeneza ya kuzidisha ile ndo naonaga miyeyusho… naona kama siku unaweza ukachokwa
List ya wasanii ambao wanamchekesha na anaenjoy kuwa nao ni hii; “Barnaba, Baba Levo, AT ndo namba moja. Kama mnasafiri unaenjoy safari nzima…
Mkasi V
Mkasi VI